Saturday, July 18, 2009

Papa afungwa POP

KIONGOZI wa Kanisa katoliki duniani, Papa Benedict XVI amefanyiwa operesheni katika mkono wa kulia kurekebisha mfupa uliovunjika.
Papa alianguka chumbani usiku wa kuamkia jana, alipelekwa hospitali saa nne asubuhi jana na akaruhusiwa saa sita baadaye.
Kiongozi huyo alitoka hospitali akionyesha kuwa mwenye afya njema, aliwapungia watu kwa mkono wa kushoto na wakati fulani alionyesha kwamba ni kwa nini aliwasalimu kwa mkono huo.
Papa amefungwa POP, inatarajiwa kutolewa baada ya mwezi mmoja.

No comments:

Post a Comment