Friday, March 6, 2009

Wema Sepetu kituko





MISS Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu jana alikuwa kituko baada ya mama yake mzazi, Mariam Sepetu kumdhamini kwa sh 500,000 katika mahakama ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Katika kile kinachotafsiriwa kuwa ni kukosa adabu, Wema alimuacha mama yake mzazi na kwenda kumkumbatia mwanaume anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, Jumbe Yusuph.

Mariam alikwenda kumtoa kwa nguvu mwanae kwa mwanaume huyo na kuondoka naye.

Leo asubuhi kulikuwa na mjadala mkali ofisini kuhusu alichokifanya wema, baadhi wanawatuhumu wazazi wake kuwa wamechangia kuwa alivyo, wengine wanasema ni hulka yake.
Wema ameshitakiwa kwa tuhuma za kuvunja kioo cha gari la aliyedaiwa kuwa alikuwa mpenzi wake, Stephen Kanumba chenye thamani ya sh 1,000,000.

No comments:

Post a Comment