KILA ninapousikia wimbo huu ulio katika mahadhi ya mnanda huwa nafikiria mengi hasa yale yanayotokea katika maisha yetu ya kila siku. Baadhi ya maneno katika wimbo huo ulio kwenye chati hivi sasa ni
Usinione mzembe, kupata ni majaliwa
Ndevu amenyimwa ng'ombe lakini mbuzi kapewa
Kwa Mungu hauna hisa ila umetunukiwa
Hautazikwa na pesa au gari ulilonunua
Hizo nyumba za kisasa wapo watakaochukua
Uliyetafuta naye kuni ndiye wa kuota naye moto
Kwa mtazamo wangu maneno hayo hapo juu ni ya kweli, wewe unasemaje?
No comments:
Post a Comment