Saturday, March 28, 2009

Polisi watuhumiwa kumuua dereva wa teksi


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova

POLISI mkoani Dar es Salaam wanatuhumiwa kumuua dereva wa teksi kwa kumpiga risasi.

Inadaiwa kuwa polisi walimsimamisha dereva huyo aliyekuwa akiendesha teksi, alisimama, wakamuamuru afungue vioo alikataa, wakakivunja na kumpiga risasi akafa.

Mkuu wa Mkoa huo, Abbas Kandoro ameunda tume ya watu watano kuchunguza tukio hilo.

Kandoa amemtaja polisi aliyefyatua risasi hiyo kuwa ni, Koplo Aderbert Sangu, yupo polisi kwa tuhuma za mauaji.

Miaka michache iliyopita polisi mkoani humo waliwaua wafanyabiashara watatu wa madini na dereva wa teksi mmoja kwa tuhuma kwamba ni majambazi.

Rais Jakaya Kikwete aliuamuru iundwe tume kuchunguza ikabainika kwamba hawakuwa majambazi, kesi inaendelea Mahakama kuu Tanzania.

No comments:

Post a Comment