Saturday, March 7, 2009

Mke wa Tsvangirai afa ajalini




MKE wa Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai(56) amekufa jana jioni katika ajali ya gari nchini humo.
Susan(50) alipoteza uhai baada ya gari lililokuwa likiendeshwa na mumewe kugongana na lori na kupinduka mara tatu.
Waziri Mkuu wa Zimbabwe alikuwa akiendesha gari hilo, Toyota Landcruiser kwenda kijijini kwake, Burego kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa wiki.

Ajali hiyo imezua maswali mengi, mengi yanazungumzwa lakini pia unaweza kujiuliza kwa nini Waziri Mkuu anaendesha gari mwenyewe, na bila kuongozwa na gari la polisi tena bila kuwa na walinzi?
Susan alikufa kwenye eneo la ajali, mumewe ameumia kichwani, shingoni na anapata maumivu kifuani.
Hadi leo asubuhi Tsvangirai alikuwa hospitali, Rais Robert Mugabe amekwenda kumjulia hali.

Tsvangirai na Susan walifunga ndoa mwaka 1978, Mungu kawajaalia watoto sita.

Pole kwa wananchi wa Zimbabwe kwa msiba huo, Mungu ailaze roho ya marehemu Susan mahala pema peponi, Amen.

No comments:

Post a Comment