Saturday, March 14, 2009

Hakimu ajitoa kesi ya Liyumba

KATIKA hali isiyotarajiwa, Hakimu Khadija Msongo amejitoa katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Benki Kuu Tanzania, Amatus Liyumba.

Liyumba na aliyekuwa Meneja Miradi wa BOT kwa pamoja waanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya hivyo kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 120.

Hakimu Msongo amesema amejitoa kwa kuwa ameona kuwa wananchi wanalalamikia mwenendo wa kesi hiyo na amri anazozitoa.

Februari 17 mwaka huu Msongo alimpa Liyumba dhamana yenye utata kwa kuwa awali, washitakiwa hao walitakiwa kuwasilisha mahakamani Sh bilioni 55 kila mmoja au hati za mali zisizohamishika zenye thamani hiyo lakini akapata kwa kuwasilisha hati ya mali yenye thamani ya sh milioni 882.

No comments:

Post a Comment