MMOJA wa waumini waliohudhuria Baraza la Maulid jana, alimzaba kibao Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi.
Kijana huyo, Ibrahim Said(26) alikwenda jukwaani wakati Mwinyi anahutubia waumini, akajifanya anatengeza jirani na Mzee Ruksa, akamzaba kibao.
Tukio hilo la aina yake lilisababisha mzee Mwiny ashikwe na butwaa, lakini baadaye alisema amemsamehe.
Taarifa zilizopatikana Dar es Salaam zilibainisha kwamba, kijana huyo alizaliwa Dar es Salaam, anaishi jijini humo, ni mwalimu wa tuition.
Alimaliza kidato cha sita katika shule ya wavulana Tabora mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment