WATOTO waliozaa pacha wawili wamesema, watakuwa wazazi wazuri na wataendelea na masomo.
Watoto hao raia wa Uingereza, Sammii Humphries na Daniel Sargent wanasoma pamoja, walianza uhusiano wakati wakiwa na umri wa miaka 13.
Daniel amesema, atasoma ili aje kuwa polisi, Sammmii amesema anapenda kuja kuwa muuguzi.
Sammiii alipata ujauzito wakati akiwa na umri wa miaka 14, hakugundua hadi mimba ilipofikisha wiki 22.
Hivi karibuni, mtoto mwenye umri wa miaka 13, Alfie aliibuka kuwa baba, na kama kipimo cha DNA kitathibitisha kweli ni mwanae atakuwa ni baba mwenye umri mdogo zaidi nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment