Thursday, February 26, 2009

Ivory Coast wanajuta kutufahamu


TIMU ya soka ya taifa, maarufu kwa jina la Taifa Stars jana usiku walitupa raha Watanzania kwa kuinyuka timu ya Ivory Coast bao moja kwa mzunguko hivyo kuwang'oa wenyeji hao kwenye michuano hiyo inayoshirikisha nchi nane.

Mrisho Ngassa jana alikuwa mwiba kwa Ivory Coast na ndiye alifunga bao hilo kqwa kichwa katika dakika ya 37 ya mpambano huo ulioonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya taifa, TBC1.
Maximo boys wanastahili sifa, tangu mwanzo wa mchezo walionyesha dhamira ya kutaka kushinda, walicheza kwa kujituma kutetea nchi yao.

Stars wakiinyuka Zambia watatinga nusu fainali, kila la heri vijana wa Maximo, fanyeni kweli na wengine wajute kutufahamu.

No comments:

Post a Comment