
MUDA mfupi uliopita nimepata nyepesi kuhusu aina mpya ya utapeli jijini Dar es Salaam ambao pia unahatarisha maisha ya raia wasio na hatia.
Kuna wajanja fulani wanaotumia fursa ya kwamba kila anayepigiwa kelele za Mwizi Mwizi Mwizi hadharani atasulubiwa bila ya kuhojiwa, wamezua mtindo wa kuwaomba watu simu zao, wajifanye wanabip.
Ukiwapa simu wanapigiwa na yule waliyembip ambaye ni mwizi mwenzake, wanawaomba waliowapigia wawatajie namba ya simu waliyoitumia - kwa kuwa ni washirika wenzao katika dili - ili baadaye wanadai kuibiwa simu.
Katika purukushani ya kumtafuta Mwizi huyo wa simu, ambaye si mwizi, ila yule ambaye anayedai kuibiwa ndiye mwizi halisi, inatajwa namba ya simu inayodaiwa kuibwa. Inapolia, inaita kwa mtu ambaye si mhusika, hapo hapo anaanza kusulubiwa bila kuhojiwa.
Uovu huu wa kuwahukumu watuhumiwa badala ya kuwapeleka katika mamlaka husika wakajibu tuhuma zinazowakabili umeanza kuwaathiri raia wema. Hii ndiyo bongo, kaeni chonjo, msije kuitwa wezi mkachomwa moto.
Ushauri: Mtu usiyemfahamu akikuomba simu yako ili abip kataa kata kata, mwambie simu yako haibip hata siku moja, anakushusha hadhi! Akisema si wewe unayebip, unamwambia hata kama si wewe! Akileta za kuleta unamkata kibano cha nguvu na kumpigia kelele za Mwizi Mwizi, wamsulubu yeye!
No comments:
Post a Comment