Rais John Magufuli amesema, Watanzania masikini wamechoshwa na machungu ya ugumu wa maisha, wamechoka kuwa wachungu, umefika wakati sasa nao wawe watamu.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam muda mfupi uliopita kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu 'fly overs'.
Amewaeleza wananchi kuwa, amedhamiria kupambana na umasikini unaowakabili wananchi, na kwa kuwa wanamuombea, hakuna litakaloshindikana.
Rais Magufuli pia amewaagiza viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wahakikishe jiji linakuwa safi.
Amesema, anataka Dar es Salaam iwe kama Ulaya.
Rais Magufuli ameagiza zitungwe sheria ndogo za kuwabana watu wanaochafua mazingira wakiwemo wanaotupa takataka ovyo.
No comments:
Post a Comment