“Siyo lazima uwe mtoto wa tajiri ndiyo uoneshe kipaji chako. Hili peke
yake linanipa sababu ya ziada ya kwa nini nitamani kuota kuwa Rais –
nataka niwe mfano hai wa mafanikio ya Ndoto ya waasisi wa Taifa letu,
kuwa sote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tuna haki na fursa
sawa bila kujali nani anatokea familia ipi.”
“Ndiyo maana, natangaza rasmi sasa kuwa ninatia nia ya kugombea Urais wa
Tanzania mwaka 2015,” alisema na kuamsha hoihoi, nderemo na vifijo
kutoka kwa wafuasi wake.
“Mimi ninaamini kwamba, kama hata mimi nimefika hapa kutokana na kuishi
maisha ya kimasikini, ya kuuza karanga na samaki mitaani, ya kwenda
shule pekupeku, basi kila mtanzania anaweza, na ana haki ya kufika hapa
na kwenda mbele zaidi yangu. Mafanikio siyo haki ya wachache, ni tunu ya
Mwenyezi Mungu kwa kila mtu. Ninaamini ni haki ya kila mtanzania kuota
ndoto yake, kuifanyia kazi na kuifikia,”
Dk Hamisi Kigwangalla
No comments:
Post a Comment