Picha hiyo aliipiga Rais Uhuru Kenyatta kwa kutumia simu ya mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Citizen, Jacque Maribe, baada ya mahojiano na kiongozi huyo kwenye makazi yake, Nairobi.
Kabla ya kupiga picha hiyo, mtangazaji alimuuliza Rais Kenyatta kama anaweza kupiga picha akajibu kuwa anaweza, akapewa simu, akapiga picha ya kwanza, walipoiangalia, mwandishi huyo akamweleza Rais kuwa alikuwa hajatabasamu, kiongozi huyo akapewa simu tena, akapiga nyingine mbili ikiwemo hiyo hapo juu.
Nilipenda namna kiongozi huyo alivyokuwa wakati wote wa mahojiano, alikuwa huru kuzungumzia maisha yake ya kawaida ikiwa ni pamoja na kusema kila siku anaamka saa 12 asubuhi, alisema pia anachofanya baada ya kuamka.
Kwa mujibu wa Rais Kenyatta, anapenda kula UGALI na NYAMA CHOMA na kwamba, mapenzi yake kwa vyakula hivyo kayatabadilika.
No comments:
Post a Comment