Wednesday, February 5, 2014

Rais Kikwete akutana na mhifadhi wa Sokwe Dkt.Goodall

Rais  Dkt.Jakaya Kikwete akimsikiliza mhifadhi wa Sokwe wa kimataifa  Dkt.Jane Goodall wakati mhifadhi huyo alipomtembelea Rais Ikulu na  kumwelezea kazi zake mbalimbali za uhifadhi nchini.
 
Dkt.Goodall  anajihusisha na uhifadhi wa Sokwe katika hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma  na kazi yake imeipatia Tanzania umaarufu mkubwa Duniani.
 
Dkt. Goodall ni mwanzilishi wa taasisi ya Jane Goodall Institute inayojihusisha na uhifadhi wa Sokwe.
 
 Picha na Freddy Maro

No comments:

Post a Comment