Monday, December 2, 2013

Miss Tanzania USA

 
Mlimbwende Joy Kalemera akipungia mashabiki baada ya kushinda mashindano ya Miss Tanzania USA Pageant yaliyofanyika usiku wa Jumamosi Novemba 30, 2013 kwenye ukumbi wa Hollywood Ballroom uliopo Silver Spring , Maryland na Mhe. Balozi Liberata Mulamula ndiye aliyekua mgeni rasmi.

Balozi Liberata Mulamula akiwa mwenye furaha baada ya shindano hili kufana sana na kuandika historia iliyobeba ukurasa mpya wa kutangaza Tanzania kwenye mashindano haya ya Miss Afrika USA Pageant ambayo Tanzania ilikua na mshiriki wa kwanza mwaka huu ambae ushiriki wake haukupitia ngazi hii.

Joy Kalemera akipongezwa na washiriki wenzake waliokua nae kwenye kinyang'anyiro hiki kilichoanzia miezi miwili iliyopita.

Balozi Liberata Mulamula akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa kwanza katika historia ya Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera kulia ni Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant Ma Winny Casey.

 Joy Kalemera katika picha ya pamoja na majaji pamoja na mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant, Lady Kate (kulia)

Kutoka kushoto ni Faith Kashaa kutoka Alabama ambaye ndiye mshindi wa tatu, Doreen Rumaya kutoka Pennsylvania mshindi wa pili, Joy Kalemera kutoka New Jersey Miss Tanzania USA Pageant, Julia Nyerere mshindi wa Tano na Namala Elias mshindi wa nne wakiwa kwenye picha ya pamoja
 Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na washiriki wenzake.
 
Kwa hisani ya Blog ya Swahilivilla

No comments:

Post a Comment