Familia ya Isaack Mruma (wa tatu kushoto) ikiwa kanisani katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Mbezi Beach, Dar es Salaam.Wa kwanza kushoto ni mama mzazi wa Jerry, Joyce, kaka wa Jerry, Khan na mdogo wa Jerry, Kelvin.
Isaack Mruma akimfariji mkewe Joyce Mruma kwa msiba huo wa mtoto wao.
Kelvin anamfariji mama yake
Isaack Mruma akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mtoto wake Jerry Mruma.
Mama mzazi wa Jerry, Joyce akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mwanae.
Kijana Jerry Isaack Mruma (23) alikuwa anasoma Chuo
Kikuu cha Kimataifa cha Marekani (USIU) tawi la Nairobi nchini Kenya akichukua Shahada ya
Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA) aliuawa wakati akitoka kwenye hafla ya
usiku wa Mtanzania mjini Nairobi. Mwili
wake ulipatikana mwishoni mwa wiki iliyopita. Amezikwa jana katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Cleopa Msuya (kulia) akimfariji Isaack Mruma kwa msiba wa mtoto wake.
Cleopa David Msuya akimfariji mama wa Jerry, Joyce kwa msiba wa mwanae.
Isaack Mruma na mkewe, Joyce wakiweka udongo kwenye kaburi la mtoto wao Jerry.
Isaack Mruma na mkewe
Joyce Mruma wakiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wao Jerry Mruma. picha zote kwa hisani ya blog ya Father Kidevu
No comments:
Post a Comment