Thursday, November 21, 2013

Mauaji DSM- Majeruhi aaga dunia Muhimbili

1424343_755264624500789_596758088_n
Kijana aliyeua watu kwa risasi, Gabrieli Munisi


 Christina alikuwa mpenzi wa Gabrieli Munisi.

MAJERUHI wa tukio la mauaji yanayohusu mapenzi, raia wa nchi jirani ya Kenya, Francis Shumila, amefariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam.
 
Inadaiwa kuwa, Mkenya huyo alikuwa mchumba mpya wa msichana anayeyedaiwa kuwa chanzo cha mauaji hayo, Christine Alfred Newa.
 Mlengwa mkuu wa shambulizi hilo, Christina Newa akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwao, Ilala, Dar es Salaam.
 

Juzi asubuhi, mchumba wa zamani wa Christina, Gabrieli Munisi alimpiga risasi kijana huyo kichwani na kifuani, naye akajiua hapo hapo Ilala Amana.

Munisi aliwapiga risasi watu wanne; Christina, Francis, mdogo wake Christina, Alpha Alfred aliyekufa papo hapo na mama mzazi wa binti huyo, Hellen Alfred.
Mama mzazi wa marehemu Alpha Newa akifika nyumbani baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali (Picha na blog ya HabariMseto).
Alpha ameacha watoto wawili akiwemo mmoja wa miezi minane.Mama huyo alikuwa anafanya kazi katika benki.
 Dada wa Christina, Carolyne Newa akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwao, Ilala, Dar es Salaam.

Kaka wa Alpha, Aloyce Newa, amesema Christina anasoma Shahada ya Uzamili ya Telecommunication katika visiwa vya Cyprus na si kwamba alikuwa akienda kwenye starehe na Francis.


Aloyce alikiri ni kweli Munisi alikuwa na uhusiano na Christina, lakini akadai uhusiano huo uliisha muda mrefu. 
 
Amesema, Alpha, alikuwa akiishi Zanzibar akiwa na mumewe na watoto wake wawili; mmoja wa miaka saba na mwingine wa miezi minane na alifikia katika nyumba hiyo ya familia kikazi.

Alisema gari lililokuwa linatumiwa ni la Alpha na dereva ni shemeji yake, ambaye mara nyingi amekuwa akimuendesha awapo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment