Kijana Mtanzania aliyeuawa jijini Nairobi nchini Kenya, Jerry Mruma (23) anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwili wa Jerry, uliletwa jana kutoka Kenya.
Marehemu ni mtoto wa aliyekuwa Mhariri
Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers (TSN), wachapishaji wa magazeti
ya Daily News, Sunday News, HabariLeo, HabariLeo Jumapili na SpotiLeo,
Isaac Mruma.
Jerry alikuwa mwanafunzi wa shahada ya Uzamili, na pia
alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kilimo Yetu jijini Nairobi,
inayojishughulisha na masuala ya kilimo.
Buriani Jerry.
No comments:
Post a Comment