Friday, October 18, 2013

Walivyomzika mama wa Ufoo Saro

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Anastazia Saro likiwekwa kaburini.
Mkuu wa jimbo la Hai, Aminirabi Swai akiongoza ibada ya maziko katika makaburi ya kanisa hilo na kisha kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Anastazia Saro.
Mkuu wa jimbo la Hai,Aminirabi Swai akiongoza ibada ya maziko katika makaburi ya kanisa hilo na kisha kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Anastazia Saro.
Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga akiweka shada la Maua katika kaburi.
Mtoto Alvis Anthery akiweka shada la maua katika kaburi la Bibi yake marehemu Anastazia Saro.(picha na Dixon Busagaga).

 Msemaji wa familia Allelio Swai amesema, Anastazia Saro alifikwa na mauti hayo baada ya kupigwa risasi na mkwewe Anthery Mushi ambaye alikwenda nyumbani kwa mama huyo eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Alisema taarifa ya madaktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), inaonyesha,Anastazia Saro alikufa baada ya kushambuliwa kwa risasi tano.

“ Ufoo taarifa ya madaktari inaonesha alichanika utumbo mkubwa na kiasi utumbo mdogo,lakini tunashukuru hali ya Ufoo inaendelea kuimarika ,lakini maombi yenu yanahitajika ili aweze kurejea katika hali yake ya zamani ,na aweze kulitumikia taifa kwa kuhabarisha “alisema Swai.

Baba mdogo wa Ufoo Saro, mzee Eshikaeli Saro, akizungumza katika ibada ya mazishi kanisani hapo,alisema familia na kanisa imepoteza mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya jamii na kanisa.

“Mama alikuwa ndiye mpambaji wa madhabahu ya kanisa ,na alihakikisha kanisa linakuwa katika hali ya usafi kabla ya ibada na hata pale wanakwaya walipokuwa na mazoezi ya kutwa hapa kanisani alihakikisha wanapata chakula”alisema Saro.

Kwa hisani ya blog ya Lukaza

No comments:

Post a Comment