Tuesday, October 29, 2013

Walivyomzika Kamanda James Kombe

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, kanda ya Kaskazini, Dkt. Martin Shao akiendesha Ibada ya Maziko ya  aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyefariki dunia Oktoba 21 mwaka huu, Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akitoa heshima za mwisho katika jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe.
Mkuu wa wilaya ya Hai, Novatus Makunga (kushoto) na Mkuu waWilaya ya Moshi, Dkt. Ibrahimu Msengi wakitoa heshima za mwisho katika jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe.
Kamanda wa Polisi mkoanbi Kilimanjaro, ACP-Robert Boaz akitoa Salamu za Rambirambi kwa niaba IGP Said Mwema katika ibada ya Maziko ya aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe
Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Aisha Nyerere, akitoa heshima za mwisho katika Jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe
Mke wa Marehemu, Maria Kombe (katikati) pamoja na watoto wake wakifuatilia ibada ya maziko.





Mke wa Marehemu, Maria Kombe, akiweka Ua katika Kaburi la marehemu mume wake, aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.

Watoto wa Marehemu Kombe, wakiongozwa na Kaka yao, Dustan Kombe kuweka  Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.


  Polisi wakitoa heshima za mwisho katika kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. 
 
Picha zote na Taifa Letu.com blog

No comments:

Post a Comment