Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV, ufoo Saro bado yupo hospitali, Muhimbili, kafanyiwa opereshi ya kutoa risasi mwilini.
Ufoo alipigwa risasi jana, na katika tukio hilo mama mzazi wa mwandishi huyo aliuawa kwa risasi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni alisema jana kuwa, tukio hilo lilitokea jana alfajiri nyumbani kwa mama mzazi wa mwandishi huyo.
Kwa mujibu wa kamanda Wambura, mwanaume huyo anafanya kazi Umoja wa Mataifa (UN) nchini Sudan.
Kamanda
Wambura amesema, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao, walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi
wa Ufoo Saro (mama mkwe) na ndipo mwanaume huyo alipomshutumu mama mkwe
wake kwamba anamtetea mwanae, akatoa bastola na kumpiga mama huyo risasi kichwani na kumuua papo hapo.
Baada ya hapo alimpiga
Ufoo risasi ya mbili moja ya tumboni na ingine ya mguuni na kudhani
kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya
kidevuni na kufa hapo hapo.
No comments:
Post a Comment