Sunday, October 20, 2013

Julius Nyaisanga afariki dunia

Kuna taarifa kutoka Morogoro kuwa, Mtangazaji Mkongwe nchini, Julius Nyaisangah 'Uncle J' amefariki dunia leo asubuhi. 

Nyaisangah alikuwa Mhariri Mtendaji wa Abood Media iliyopo mkoani Morogoro na aliwahi kufanya kazi Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na Redio One ambapo alikuwa Mkurugenzi. 

Inadaiwa kuwa, mtangazaji huyo alikuwa akiugua kwa muda mrefu. 


No comments:

Post a Comment