Serikali ya Kenya imesema, vikosi vya uokoaji vimeua magaidi mawili na vimeokoa takribani mateka wote waliokuwa wametekwa na magaidi katika jengo la maduka la Westgate jijini Nairobi tangu Jumamosi mchana.Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya, Joseph ole Lenku amesema, kazi
ya kuokoa mateka katika jengo hilo karibu
inakwisha.
Amewaeleza
waandishi wa habari kwamba, magaidi wote ni wanaume, lakini baadhi yao wamevaa nguo za kike, na kwamba, wanakadiriwa kuwa kati ya 10 hadi 15.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, waokoaji wamewazingira magaidi
waliojificha kwenye maduka yaliyopo kwenye jengo hilo kubwa na watawasambaratisha.
Kwa
mujibu wa Waziri Lenku, hadi sasa magaidi wawili wameuawa, wenzao wamejeruhiwa, na kwamba, askari 10 wamejeruhiwa katika mapambano na magaidi hao.
Amesema, moshi unaotoka kwenye
jengo hilo unatokana na kitendo cha magaidi hao kuchoma magodoro ili
kuharibu mipango ya wanajeshi kuokoa mateka.
No comments:
Post a Comment