Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema
Watu watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Mwanza wakituhumiwa kuhusika kumuua Kamanda wa Polisi mkoa huo, Liberatus Barlow.
Watuhumiwa hao ni Muganyizi Michael (36) mkazi wa Nyakabung; Magige Marwa
maarufu kwa jina la “Tatoo”(48), mkazi wa Bugarika; Chacha Mwita (50) mkazi wa
Gongolamboto Dar es Salaam; Buganze, Edward Luseta (22), mkazi wa
Tandika na Bhokle Mwita (42) mkazi wa Ukonga Mombasa, Dar es Salaam.
Wanadaiwa kuhusika kumuua RPC Barlow, usiku wa Oktoba 13, mwaka huu eneo la Minazi Mitatu
Kitangiri wilaya ya Ilemela.
Watuhumiwa
wengine watano akiwemo Mwalimu Doroth Moses Lyimo aliyekuwa na Kamanda
Barlow wakati tukio hawakufikishwa mahakamani.
Watu wengine waliokuwa wakishikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na mauaji ya Barlow, lakini hawakufikishwa mahakamani
ni Felix Felician (50), Philemon Felician maarufu kama “Fumo” (46) aliyewahi kuzichezea
klabu za Pamba ya Mwanza na Yanga ya Dar es Salaam ambaye pia ni mdogo wa Felix, Bahati Lazaro (28) na Amos Woibe Mabhoto maarufu kama
“Bonge” (30), wote wakazi wa jijini Mwanza.
|
No comments:
Post a Comment