Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred
Miss Tanzania 2012, ni Brigitte, kapata zawadi ya gari aina ya Noah, na fedha sh milioni 8.
Nyota ya mrembo huyo ilianza kung’aa tangu kitongoji cha Sinza, alitwaa taji la Sinza
na baadae akafanya kweli kwa kutwaa taji la Redds Miss Kinondoni.
Si hivyo tu, binti huyo alidhihirisha ukali wake
baada ya kuwabwaga warembo wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo
kutoka kanda mbambali.
Mpinzani mkubwa wa Brigitte alikuwa mrembo
kutoka Kanda ya Ziwa, Miss Mara ambaye pia ni Miss Kanda ya Ziwa, Eugene Fabian.
Enagene alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika shindano hilo kubwa
ambalo Brigitte ameondoka akiendesha gari aina ya NOAH na kitita cha
Shilingi Milioni 8.
Nafasi ya tatu imekwenda kwa Miss Kigamboni na
Miss Temeke 2012, Edda Sylvester.
Mrembo wa Dar Indian Ocean, Magdalena Roy amekuwa wa nne, na nafasi ya Tano
ikaenda Kanda ya Ziwa tena kwa Miss Mwanza, Happyness Daniel.
Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati) akiwa na washindi wa pili, Eugine Fabian na mshindi wa tatu, Edna Sylvester
Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred akiwa na mama yake , Vardiana Augustine Mashingia
Zawadi kwa Miss Tanzania 2012
No comments:
Post a Comment