Mama mzazi wa mtoto aliyekatwa mkono baada ya kuteswa. |
Mtoto Aneth akiwa hospitalini |
Mama mzazi wa mtoto Aneth akiongea na mwandishi wa habari hospitalini |
MAMA mzazi wa mtoto Aneth Johanes (4), Asera Mkandara amewashukuru wananchi waliosaidia kutoa taarifa na hatimaye kuokoa maisha ya mwanaye aliyekuwa
akiishi kwa mateso.
Mtoto huyo , amekatwa mkono ikiwa ni sehemu ya tiba kutokana na mateso ya shangazi yake. Aneth ni mtoto wa pili kwa mama huyo, mwingine ana umri wa miaka 7, anaishi na bibi yake mjini Bukoba.
Mama huyo anayeishi Muleba mkoani Kagera amesema, alipata taarifa
za tatizo ya mwanawe lakini hakufafanuliwa ni tatizo gani.
Mshitakiwa kwenye kesi ya kumtesa mtoto Aneth |
Imedaiwa mahakamani kuwa, mwanamke huyo alimfungia ndani mtoto Aneth ndani na kumchoma kwa maji ya moto
Mama wa mtoto Aneth anashukuru kukuta mwanaye ni mzima na anawashukuru madaktari waliompa msaada kwani inawezekana huduma za matibabu zingechelewa angeweza kupata madhara makubwa zaidi.
Kwa hisani ya blog ya Mbeya Yetu
Mwendesha mashitaka wa Serikali,
Achiles Mulisa ameiambia Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24) alitenda
kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu
mtoto Aneth.
Mulisa amesema, kosa hilo ni
kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha 222(a) sura ya 16 kama
ilivyorejewa mwaka 2002.
Mshitakiwa
amekana shitaka hilo ambapo amerudishwa mahabusu hadi Novemba 22, Mwaka huu
kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mama wa mtoto Aneth anashukuru kukuta mwanaye ni mzima na anawashukuru madaktari waliompa msaada kwani inawezekana huduma za matibabu zingechelewa angeweza kupata madhara makubwa zaidi.
Kwa hisani ya blog ya Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment