Friday, November 2, 2012

Breaking News: Lori la mafuta laua chekechea wawili Mbeya

KUNA ajali imetokea Mbeya, lori la mafuta limewagonga na kuwaua watoto wawili wanafunzi wa shule ya awali (Chekechea)

Dakika chache zilizopita, Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Kwa mujibu wa RPC Athumani, watoto hao walikuwa wanavuka barabara leo asubuhi kwenda shuleni, wakagongwa na kufa papo hapo. 

Wananchi kwenye eneo hilo wameweka mawe na magogo barabarani kuzuia magari yasipite, wanashikiza yawekwe matuta.

 



Watoto hao wamegongwa katika barabara kuu itokayo Zambia kwenda Dar es Salaam.

Vijana wameweka mawe na magogo barabarani kuzuia magari yasipite na wanashinikiza yawekwe matuta kwenye eneo hilo


No comments:

Post a Comment