Monday, August 13, 2012

Walivyompokea Dk Steven Ulimboka Dar es Salaam


 Mamia ya watu wakimpokea Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitoka Afrika Kusini alipokuwa akipata tiba baada ya kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande, Dar es Salaam Juni 26,2012.
 
Picha ya chini ikimuonesha Dk. Ulimboka akiwa katika hali mbaya baada ya kuokotwa katika msitu wa Juni 27.

 Wanaharakati wakipaza sauti wakati wanampokea Dk. Steven Ulimboka.
 Dk. Ulimboka akiwapungia mkono wananchi waliokwenda kumpokea
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka akiwa ameshika ua mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, akitoka Afrika Kusini kwa matibabu
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka akiwa ameshika ua mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, akitoka Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kutekwa, kuteswa Juni 26, 2012 na kutupwa katika Msitu wa Pande, Dar es Salaam.
  Wanaharakati pamoja na madaktari wakisukuma gari alilokuwa amepanda Dk Ulimboka mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment