Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Agosti 1 mwaka huu) ametangaza
kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya mechi ya kirafiki itakayochezwa
ugenini Agosti 15 mwaka huu.
Wachezaji
walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
wanatakiwa kuripoti kambi kwenye hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam,
Agosti 8 mwaka huu saa 1 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku
inayofuata.
Makipa
walioitwa kwenye kikosi hicho ni Deogratias Munishi (Azam), nahodha
Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha msaidizi
Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na
Shomari Kapombe (Simba).
Viungo
ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi (Simba),
Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo (Azam),
Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa
Sugar).
Wachezaji
wanaounda safu ya ushambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP
Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga),
Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo- DRC).
No comments:
Post a Comment