Hivi
majuzi niliskia kuwepo kwa tuzo za waandishi wa habari za mtandaoni
maarufu kama waandishi wa magazeti tando (blogs).
Katika Tuzo hizo
ambazo ziliandaliwa kwa vigezo wanavyovijua Vodacom, wametajwa washindi
fulani.
Kama mdau wa kawaida katika magazeti tando, miongoni mwa waasisi
wa Bloger wa kwanza kabisa wa Kitanzania naamini kwa sasa kama nchi hii
itakuwa inaendeshwa kishkaji, kirafiki, kima kundi na ikaachwa bila
kukemewa basi siku si nyingi tutapoteza ladha ya mashindano yanayopima
viwango na ubora wa kazi hali itakayofanya nchi kubakia kuwa ya
wababaishaji kila siku.
Eneo
hili la magazeti tando niliwahi kulilalamikia kutokana na kukosekana
ubunifu hasa inapotokea habari moja inajaa kila blog kama ambavyo ipo
katika magazeti ya Tanzania.
Kwa kuona hili hili nashangaa blog iliyo na
kazi ya kubandika picha za magazeti ya kila siku ama habari za wasanii
walio nje au kuchota mawazo ya watu katika FB na twitter, au kusubiri
taarifa za Maafisa Habari ikaibuka mshindi kwa kuwa tu eti inaonesha
kuwa na wasomaji wengi.
Kwamba hamjui kuwa ukiseti weblog yako ihesabu
wanaoitembelea itahesabu bila kujali ni nani anaingia mara ngapi?
Kwa mantiki hii kigezo cha idadi ya watu si kigezo kuonesha kuwa huyu ni mahiri katika kutoa taarifa katika Blog yake.
Natoa
rai, kuwa mliopata nafasi ya kuwa na nguvu katika makampuni msitumie
nafasi hizo vibaya kwa kutaka kuidhinisha udhamini wa blog kwa rafiki
zenu na kisha kupoteza ladha ya ubunifu katika blog.
Najua mmefanya hivi
sana katika maeneo kama ya sanaa za urembo na kwingineko lakini
kumbukeni hili limezidi na haliwezi kuvumiliwa!
Jamhuri hii ilikuwepo
kabla yenu na hiki mnachojivunia kwa kuwa kimetengenezwa na urithi wa
Baba zenu msitarajie kitabaki kuwa hivi kila siku.
Tendeni haki japo
kidogo jamii hii itawaheshimu.
Kwa masikitiko na hasira kidogo nawasilisha!
Bonny Makene Road to PhD.
No comments:
Post a Comment