Mahakama Kuu Kanda ya Tabora leo imemvua ubunge, Mbunge wa Igunga, Dalaly Peter Kafumu (CCM).
Jaji Mary Shangali wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, ametangaza kutengua matokeo hayo
baada ya kuridhika na hoja saba kati ya 17 zilizowasilishwa hapo na upande wa
mlalamikaji.
Mlalamikaji katika kesi
hiyo ni aliyekuwa mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye katika uchaguzi uliofanyika
Oktoba 2 mwaka jana, kuziba nafasi ya Rostam Aziz wa CCM aliyejiuzulu nafasi
zote za uongozi ndani ya CCM.
No comments:
Post a Comment