Rais
Dkt.Jakaya Kikwete akimkabidhi Mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere Tuzo ya Juu ya
Heshima ya Taifa la Burundi aliyotunukiwa hayati Mwalimu
Julius Nyerere wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Burundi
yaliyofanyika mjini Bujumbura wiki iliyopita.
Mwalimu Nyerere alitunukiwa
tuzo hiyo kwa mchango wake wakati wa harakati za kupigania uhuru wa
Burundi ambapo alikuwa mshauri wa karibu wa Waziri Mkuu wa Kwanza wa
nchi hiyo Prince Louis Rwagasore.
Rais Kikwete alimkabidhi Mama Maria
tuzo hiyo leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha Freddy Maro).
No comments:
Post a Comment