Wednesday, July 18, 2012

Breaking News- Meli yazama ikiwa na abiria 200

Kuna taarifa kwamba, meli ya abiria iliyotajwa kwa jina la Sky Gate imepinduka na inazama katika Bahari ya Hindi kwenye eneo liitwalo Chumbe.

Hadi hivi sasa meli hiyo imepiduka kabisa, yaani chini juu, na kuna mawimbi makubwa kwenye eneo ilipopinduka.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, meli hiyo ilikuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar, na ilikuwa imebeba abiria zaidi ya 200.


 Mwokoaji akiwa na mmoja wa maiti wa ajali hiyo
   Majeruhi wakiwa katika mgongo wa boti hiyo wakisubiri kuokolewa.
 Baadhi ya Abiria wakiwa katika moja ya chombo cha kuokolea wakielea baharini wakisubiri kuokolewa.
  Meli ya  Mv Skagit ikiwa imeshazama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250 juu ni baadhi ya waokoaji wakiwa tayari kutoka huduma ya kwanza 
 Moja ya MV SKAGIT iliyobakia ilivyo leo baada ya Nyingine kuzama
 
  Mmoja wa Majeruhi akipata huduma ya Kwanza baada ya kuokolewa akiwa katika bandari ya malindi
  Daktari akitowa huduma ya kwanza kwa mmoja wa majeruhi wa boti iliozama ikiktokea Dar-es-Salaam kuelekea Zanzibar.
 
Picha Na Haki Ngowi Blog

No comments:

Post a Comment