Askari Kanzu akipita katikati ya wanafunzi kuwakamata wanafunzi waliotajwa kuongoza vurugu hizo.
Mitihani ambayo ilikuwa ifanywe na wanafunzi kuanzia leo imechanwa
Miongoni
mwa uharibifu walioufanya wanafunzi hao kwa madai ya kukosa ubeche
shuleni hapo ni pamoja na kuvunja vunja madirisha yote ya shule hiyo na
ofisi za walimu kama inavyoonekana.
Mkuu
wa Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya Chrispine Meela akizungumza na
wanafunzi wa shule ya Manow baada ya kutokea kwa vurugu hizo.
Mkuu wa Wilaya akiwa pamoja na Uongozi wa shule hiyo ya kanisa la KKKT.
Wanafunzi 24 wa Shule
ya Seminary Manow, Iliyopo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, wanashikiliwa
na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi kufuatia vurugu na uharibifu wa mali
za shule na kanisa zilizotokea usiku wa Juni 13,2012 shuleni hapo.
Wanafunzi
hao wanatuhumiwa kufanyafanya uharibifu wa mali ya shule hiyo huku vitu
vingine vikiibiwa na jumla ya thamani ikitajwa kuwa ni Shilingi Milion
50.
Mkuu wa Shule hiyo ya Manow, Watson Masiba amesema mgomo huo ulianza mchana kwa kuwa wanafunzi hawakutaka kula Ugali baada ya uongozi kuwaarifu kuwa siku hiyo kusingekuwa na ratiba ya wali kwa kuwa mchele siku hiyo ulikuwa kidogo.
Uongozi wa shule ulipojitahidi kaandaa chakula hicho usiku huo lakini wanafunzi hao walianza kufanya vurugu kwa kuvunja vioo vya majengo na kuvunja milango na kuiba computer 11 za shule pamoja na kuingia katika chumba cha kuandalia mitihani na kuchana mitihani yote iliyoandaliwa kwa ajili ya kuanza kuifanya leo tarehe 15.06.2012.
Kwa mujibu wa maelezo ya wanafunzi na wanakijiji wanaoizunguka shule hiyo imejionyesha kuwepo kwa tofauti kati ya uongozi wa shule na wanafunzi hivyo kufikia wanafunzi hao kutafuta sababu ya kufanya vurugu kwa kiasi cha uharibifu wa mali za shule na Kanisa.
Askofu Dr Esrael Mwakyolile amesema, uharibifu ni mkubwa sana na zaidi ya mali zisizopungua shilingi milioni 50 zimeharibiwa hivyo ameitaka serikali kupitia vyombo vya dola kuchukua hatua kwa wale watakao bainika kuhusika na tukio hili kulipa fidia na uongozi wa shule uwaadhibu wahusika.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Chrispin Meela amekemea vikali kitendo kilichofanywa na wanafunzi hao ukizingatia shule hiyo ni ya kanisa la kiinjili la Kilutheri hivyo kuwa mfano wa tabia njema kuliko kuchukua hatua za Kigaidi kuharibu majengo na kuiba mali za shule.
Meela ameamuru shule hiyo ifungwe hadi Julai 02, 2012
kwa kidato cha pili, tatu, Nne na sita kwa kuwa imeonekana kuwa ndiyo
viongozi wa uharibifu huo na kwamba, wanafunzi watakaporudi shuleni hapo waende na wazazi wao, na wajieleze kwa maandishi.
www.mrokim.blogspot.com
No comments:
Post a Comment