Sunday, June 24, 2012

Uzinduzi wa filamu ya Super Star ya Wema Sepetu

Mwigizaji Wema Sepetu akiingia ukumbini wakati wa uzinduzi wa filamu yake ya Super Star aliyoizindua kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo, ikihudhuriwa na watu maarufu pamoja na wanamzuziki na waigizaji.
Wema Sepetu akipozi kwa picha mara baada ya kukaa kabla ya kuanza kuchezwa kwa Demo ya filamu hiyo usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro.
Wageni waalikwa mbalimbali wakishuhudia uzinduzi wa filamu ya Super Star iliyochezwa na mwana dada Wema Sepetu kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro
Wanamzuiki, watangazaji pamoja na waigizaji mbalimbali wa filamu waliohudhuria katika uzinduzi huo kutoka kulia ni Charles Baba wa Mashujaa Band, Hatman, Mtangazaji Benny Kinyaiya, Mchekeshaji Steve Nyerere, Muigizaj Ramond Kigosi na Richie Mtambalike "Rich Rich" wakishoo Love.
Mwanamuziki Mwinyi ambaye ndiye aliyemvisha pete ya Uchumba Wema Sepetu katika filamu hiyo naye alikuwepo.
 
Waigizaji mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo
Kundi la THT likifanya vitu vyake katika uzinduzi huo
Ankal Michuzi na maiwaifu wake kulia na rafiki yao wakipozi kwa picha
Kulia ni Asma Makau na Dina Marios wakiwa na marafiki zao katika uzinduzi huo.
 
Kwa hisani ya blog ya Lukaza
       

No comments:

Post a Comment