|
Wanafunzi
wa shule ya Msingi Etaro wakiwa darasani wakimfuatilia
mwalimu. | |
|
Wanafunzi wakiendelea na masomo yao huku wengine wakitumia magoti yao kama sehemu za kuandikia huku wakiwa wamekaa chini. |
Uhaba wa madawati katika shule za msingi
na sekondari umeendelea kuumiza vichwa vya wapenda elimu pamoja na
wazazi kwa ujumla nchini.
Upungufu wa madawati katika shule za
msingi umeendelea kudidimiza kiwango cha elimu nchini huku ukichangia
kuongezeka kwa utoro kwa kusababisha wanafunzi wengine kukata tamaa ya
kusoma na mazingira ya shule kwa ujumla ambayo si rafiki kwao.
Matokeo ya wanafunzi kukaa chini
husababisha wanafunzi kuandika wakiwa wameinama na wengine hata kulala
kifudi fudi na wengine kuchuchumaa.
|
Hali halisi ndiyo hii wilayani Musoma vijijini |
|
Wanafunzi wengine wakiyageuza madawati mabovu angalau wapate sehemu ya kukaa. | | | | |
|
Wengine wanatumia viatu vyao kukalia, na wasio na viatu wanakaa kwenye vumbi.
Chanzo: Blog ya Lukaza | | | | | | | |
No comments:
Post a Comment