Friday, June 15, 2012

Tuzo za TASWA mwaka 2011


Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akikabidhi tuzo kwa Mwanamichezo Bora wa Mwaka 2011, Shomari Kapombe wakati wa hafla ya utoaji tuzo wa Wanamichezo Bora Tanzania kwa Mwaka 2011 zilizoandaliwa na TASWA na kudhaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam Alhamisi usiku.   

Mkurugenzi Mtendaji wa The Guardian Limited, Kiondo Mshana akitangaza mshindi wa Tuzo ya Mwanariadha Bora wa Kike ambapo Zakia Mrisho aliibuka mshindi wakati wa hafla ya utoaji tuzo wa Wanamichezo Bora Tanzania kwa Mwaka 2011 zilizofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam Alhamisi usiku.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akikabidhi cheti cha Heshima kwa Rais wa TFF, Leodger Tenga ambaye alikuwa Nahodha wa timu ya  Taifa Stars iliyofanikiwa kuingia katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980.

Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto akikabidhi tuzo kwa Mwanamichezo Bora wa Netiboli, Lilian Sylidion.

Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka akikabidhi tuzo kwa Mwanamichezo Bora wa Ngumi za Kulipwa, Nasib Ramadhan.
Mpigapicha za habari Mwandamizi, Athmani Hamisi akikabidhi tuzo kwa mchezaji bora wa kiume katika mchezo wa wavu, Mbwana Ally.

Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL, Teddy Mapunda akimpongeza Shomari Kapombe.

Mchezaji wa Simba SC, Shomari Kapombe ambaye ameibuka mchezaji bora wa mwaka akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa tuzo hizo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Simba huku akiwa ameshikilia tuzo yake na mfano wa hundi yenye thamani ya milioni 12/- baada ya kukabidhiwa na Rais mstaafu Alhaj ali Hassan Mwinyi.  Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Breweries Limited, Richard Wells , (kushoto) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL, Teddy Mapunda na (wa pili kutoka kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.
Sehemu ya wanakamati ya maandalizi ya tuzo hizo.

Wanenguaji wa Bendi ya Extra Bongo wakilishambulia jukwaa wakati ilipotumbuiza katika tuzo hizo.
Picha zote na JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
Mwanamichezo Bora 2011, Shomari Kapombe     

No comments:

Post a Comment