Tuesday, June 19, 2012

Kuanzia Julai utaweza kwenda Zanzibar na gari lako






 Abiria wataweza kubarizi ubaridi na raha za pwani.


Meli ya kisasa karibuni kuzinduliwa ina uwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.

KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwa ajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja. 
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa.

Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kwa kuwa meli hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 1500, mizigo tani 500 na magari 200 kwa wakati mmoja.
Amesema, abiria atakaejisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.

Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba ana taaarifa za ujio wa meli.
Kwa hisani ya http://saidpowa.blogspot.co.uk   

No comments:

Post a Comment