Thursday, June 21, 2012

Buriani Willy Edward Ogunde


Sehemu ya wanahabari wakiwa katika majonzi.


Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd,  Dk. Reginald Mengi (kulia), akijadiliana jambo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnaye (katikati) na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),  Prof. Ibrahim Lipumba.

Mwili wa Willy Edward ukiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd,  Dk. Reginald Mengi akitoa salamu za pole.

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akitoa salamu za pole.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnaye akitoa salamu za pole kutoka Chama cha Mapinduzi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda akitoa salamu za pole.

Mpiganaji Athuman Hamis akiuaga mwili wa marehemu. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Jambo Concept, Juma Pinto ambaye ndiye aliyekuwa mwajiri wa marehemu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnaye akitoa heshima za mwisho wa Mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Marehemu Willy Edward Ogunde.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),  Prof. Ibrahim Lipumba akitoa heshima za mwisho wa Mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Marehemu Willy Edward Ogunde.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kulia), akitoa heshima za mwisho.

Umati ukisubiri kuuaga mwili wa marehemu Willy.

Mjane wa marehemu, Rehema (kushoto), na watoto wake wakiwa katika  majonzi.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Marehemu Willy Edward Ogunde.
Mwandishi wa Habari, Asha Kigundula akilia kwa uchungu huku akitulizwa na waandishi wenzake, baada ya kuuaga mwili wa Marehemu Willy Edward Ogunde. Kulia ni Somoe Ng'itu wa Nipashe.


Hali ilikua tete watu wengi walipoteza fahamu wakati wa kuuaga mwili.



Niacheni... niacheni... niacheni nimshike kwa mara ya mwisho... niacheeeeni nimshike Willy... jamani Willyyyy...........

Wahariri wakipakia jeneza lenye mwili wa Willy Edward Ogunde tayari kwa safari ya Mugumu.

Picha zote kwa hisani ya JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
Hapa ukitolewa tayari kwenda kupakia kwenye gari.    

No comments:

Post a Comment