Wakati kuna taarifa kuhusu mkazi wa Kijiji cha Magomeni Wilayani Bagamoyo Khamisi Tanga (46), aliyepata matiti kwa kile alichodai kuwa ni kutokana na kutumia ya dawa za kupunguza makati ya Virusi Vinavyosababisha Ukimwi (VVU),aina ya ARV’S , imefahamika kuwa, ni kweli kuwa dawa hizo zinakuza matiti isivyo kawaida.

Soma hapo chini simulizi ya mwanamke wa Afrika Kusini ambaye, baada ya kutumia ARV's matiti yake yamekuwa na uzito sawa wa watoto wawili wenye miaka miwili.
 
The condition, known as lipodystrophy, was recognised through changes in fat reduction or redistribution, often in one area, leading to abnormal body shape transformations.

"In 2008, my breasts started growing rapidly and got heavy, making life difficult for me," the 29-year-old woman told the newspaper.

The woman told the newspaper that in 2009 she was supposed to go for a breast reduction but could not because she was anaemic and had a bone marrow deficiency.

Doctors treated her for the anaemia and bone marrow related complications but her lipodystrophy worsened.

The woman's breasts reached her knees.

"The combined weight of my breasts is equal to carrying two two-year-old babies around at all times," she told the newspaper.

"And I cannot sleep properly because I hurt myself if I turn around carelessly."

The woman said she stayed indoors all day because she could not move.

Dr Phillip Botha from the faculty of medicine and health sciences at Stellenbosch University confirmed that lipodystrophy was a side effect of ARVs.

Health officials did not see the woman's case as a priority so she is on a waiting list for an operation at a state facility as she cannot afford the procedure herself.

Chris Hani Baragwanath Academic Hospital CEO Johanna More told the Sowetan that the hospital had more serious issues to attend to.

Gauteng health department spokesman Simon Zwane said the woman's condition was not life threatening.

"What she is asking for is a cosmetic surgical operation and unfortunately this cannot be prioritised above life-threatening and emergency surgical operations that our hospitals deal with daily," Zwane was quoted as saying.

Endelea na stori kuhusu mwanaume Mtanzania aliyeota matiti.
 
 Akizungumza na waandishi wa habari waliokwenda Wilayani humo kufanya utafiti kuhusu utekelezaji wa sheria ya Ukimwi na Chama cha Waandishi wa habari za Ukimwi(AJAT),Khamisi alisema alipatwa na mkasa huo miaka mitatu iliyopita.

Akisimulia namna alivyoanza kuugua alisema awali aliona matiti yake yakiongezeka ukubwa kila kukicha lakini hakujua kama lingeweza kuja kuwa tatizo kubwa kama lilivyo sasa.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya ilimbidi kwenda kliniki anayohudhuriaga kupata dawa na kuwaeleza manesi ambapo walimjibu kuwa imesababishwa na dawa anazotumia na hivyo kulazimika kukatizwa dozi hiyo na kupewa aina nyingine.

 Hata hivyo Khamisi alisema kwamba pamoja na kubadilishiwa dozi hajaona kama kuna mabadiliko yoyote aliyoyapata na kuongeza kwamba hivi karibuni alipewa dawa nyingine ambazo kati ya hizo kuna zile ambazo zilimsabishia matiti na tayari ameanza kupatwa na maamuvu aliyokuwa akisikiaga awali wakati matiti yalivyokuwa yanaanza kuota.

Kwa mujibu wa Khamisi ameshahangaika kupata matibabu hadi Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili lakini hadi leo hajapatiwa tiba stahili ya kumaliza tatizo hilo.

“Jamani Watanzania naomba wanisaidie kwa njia yoyote ile ili niondekane na hali hii kwani inanidhoofisha sana na kunikosesha raha hasa mbele ya wanaume wenzangu.

Kwani hapa navyoongea na nyie waandishi nilipimwa hadi kansa na matiti ndio kama hivyo mnavyoyaona yanaendelea kukua na huniuma sana hasa wakati ninapolala,”alisema kaka huyo.

Pia alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya Kikwete kumsaidia ili arudi katika hali yake ya uanaume kwa kuwa maisha kwa sasa kwake yamezidi kuwa magumu kwa kuwa hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na hali hiyo.

Kwa upande wa mtaalam wa magonjwa, Dk. Dina Komakoma,akielezea kuhusu sababu za kutokewa kwa hali hiyo kwa wagonjwa wenye maambukizi ya VVU ni jambo la kawaida japo hutofautiana.

Dk. Komakoma alisema wengine hujikuta wakinenepa au wakikonda sana na hili la Khamis sio mtu wa kwanza kupatwa na hali hiyo na kuongeza kwamba inapotokea mgonjwa akapata hali tofauti kama hiyo anapaswa kusitishiwa dawa.