RAIS Mstaafu
wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa , ametinga
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi wa zaidi ya shilingi bilioni mbili inayomkabili aliyekuwa Balozi
wa Tanzania Nchini Italia, Profesa Costa Mahalu.
Rais Mkapa amesema, kuwa ni yeye kwa
niaba ya Serikali ndiyo aliyempatia idhini Mahalu kununua jengo la Ubalozi kwa
thamani ya Euro Milioni 3 kwa njia ya mikataba miwili na kwa akaunti mbili kwa
njia ya mdomo.
Rais Mkapa
ambaye ni shahidi wa Profesa Mahalu, aliingia mahakamani hapo saa 3:45 asubuhi
akiwa amepanda kwenye gari aina VX lenye namba za usajili T 745 BQE na gari
jingine aina hiyo yenye namba za usajili T 941 BES huku akiwa akiongozwa na
walinzi na maofisa wa toka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS = Tanzania Intelligence & Security Service), ambao wengi wa
maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa walionekana kuingia katika viwanja vya
mahakama hiyo kabla ya kiongozi huyo kuwasaili, kwa tofauti tangu saa mbili
asubuhi kwaajili ya kuakikisha ulinzi wa kiongozi huyo na mazingira hayo
unaimarika.
Sekunde
chache baada ya Rais Mkapa walimuingiza katika ofisi ya Hakimu Mkuu Mfawidhi wa
mahakama hiyo, Ilvin Mugeta ambapo aliketi kwaajili ya kusuburi upande wa
Jamhuri umalize kumhoji Mahalu ndipo yeye aitwe kwenye chumba Na.9 ambacho
ndicho kilikuwa kikikutumiwa kuendeshea kesi hiyo ambayo ilifanya hadi baadhi
ya wananchi mawakili waliokuwa wakiendesha kesi nyingine kuingia ndani ya
chumba hicho kumshuhudia rais huyo akitoa ushahidi wake na wakati wote huo
maofisa wa usalama wa Taifa walikuwa wameketi ndani ya chumba cha mahakama na
kwenye mlango wa chumba hicho kilichokuwa kikiendeshea kesi kwaajili ya
kuimarisha ulinzi.
Mkapa
aliongozwa na wakili wa utetezi Alex Mgongolwa kutoa ushahidi wake alianza kwa
kula kiapo ambapo alieleza kuwa kati ya mwaka 1995-2005 alikuwa ni Mkazi Dar es
Salaam na alikuwa ndiye Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwamba
anauzoefu wa Kimataifa kwani kabla hachaguliwa kuwa
Rais aliwahi
kushika wadhifa wa Ofisa wa Mambo ya Nje, Balozi wa nchi Canada, Nigeria na
Washngton DC.
Alidai kuwa
alivyokuwa Rais wa Jamhuri alifahamu ununuzi wa jengo la ubalozi nchini Italia
na kwamba jengo hilo lilinuliwa kwa thamani ya Euro 3,098,741.40 kwa maagizo ya
serikali ambayo alikuwa akiingoza yeye na kwamba mwaka 2003 yeye ndiye
aliyekwenda mjini Rome-Italia kuzindia jengo hilo ambalo alidai ni jengo la
zuri la kisasa na wakati huo balozi alikuwa ni Profesa Mahalu na kwamba
anamfamu vyema mshitakiwa huyo.
“Serikali
yangu iliarifiwa bei na taratibu za kulinunua jengo hilo na aliyetufahamisha ni
aliyekuwa balozi wetu kule kwa kipindi hicho Mahalu.Katika manunuzi hayo mimi
kama rais wan chi nilitaarifiwa kuwa muazi wa jengo hilo alitaka malipo
yafanywe mara mbili tofauti katika akanti za muuzaji …
na serikali ilitoa baraka
zake mimi niliarifiwa na na sikuzuia na kwaniaba ya serikali yangu nikatoa
idhini jengo linunuliwe kwa mtindo huo nilioutaja hapo juu”alidai Rais Mkapa.
Yafuatayo ni
mahojiano kati ya Wakili Mgongolwa, Marando dhidi ya Rais Mkapa:
Mawakili:Katibu Mkuu Kingozi wa enzi za utawala
wako, Martin Lumbanga ambaye ni shahidi wa kwanza upande wa Jamhuri alieleza
mahakama kuwa hana taarifa kama serikali ya awamu ya tatu ilitoa kibari kwa
mshtakiwa anunue jengo hilo?
Mkapa: Ninashangaa sana Lubanga kusema hilo. Ila
mimi kama Rais nafahamu nilitoa idhini kwaniaba ya serikali ya unununuzi wa
jengo hilo kwa utaratibu ambao nimeishautaja.
Mawakili: Kama wewe rais ulijua kuwa ulitoa idhini
, inawezekana Lumbanga asiweze kujua kuwa wewe ulitoa idhini kwaniaba ya
serikali?
Mkapa: Tetee! Inawezekana Lumbanga asijue lakini
inakuwa vigumu sana.Watu akaangua vicheko.
Mawakili: Ebu soma kwa sauti hii kumbukumbu ya
Bunge “Ansard ‘ ya mwaka 2004 iliyomnukuu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa
serikali ya awamu ya tatu, Jakaya Kikwete ili mahakama isikie?
Mkapa: “Naibu Spika wizara yangu inunua jengo la
Ubalozi wa Italia , lengo likiwa kupunguza gharama za kupanga na kwamba
taratibu za sheria ya manunuzi ya umma zilifuatwa na fedha hizo zilitumwa kwa
awamu tatu ambapo mara ya mwisho kuzituma ilikuwa ni Agosti 26 mwaka 2002
ambapo jumla serikali ilituma Sh bilioni 2.9, baada ya hapo serikali ilifuata
taratibu za manunuzi na baadae ilikuja kuzuka taarifa kuhusu ubadhilifu lakini
ripoti ya CAG ,ilisema ubalozi wa Italia hakupata achafu’.
Mawakili: Je maneno hayo ya Waziri Kikwete ambaye
kwa sasa ndiye rais wa nchi katika Ansard hiyo ya bunge?
Mkapa: Maneno hayo ya Kikwete ni sahihi.
Mawakili: Wewe au serikali ya awamu ya tatu iliwahi
kupokea malalamiko toka serikali ya Italia kuwa ubalozi wetu nchini humo
ulivunja sheria kuhusu mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Hapa,kamwe sijawahi kupokea malalamiko.
Mawakili: Uwakiwa rais hujawahi kupokea malalamiko
kuwa fedha za serikali yetu zilizotumwa kwa ajili ya kumlipa muuzaji wa jengo
hilo kuwa hazijamfikia?
Mkapa: Hadi leo hii natoa ushahidi hapa
mahakamani sijawahi kupokea malalamiko ya aina hiyo.
Mawakili: Uliwahi kupata malalamiko toka kwa CAG,
Wizara ya Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi, Wazari wa Mambo ya Nje, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali wala Ofisi ya DPP kuhusu ubadhirifu wa ununuzi wa
jengo hilo?
Mkapa: Sijawahi kupata.
Mawakili: Nini ufahamu wako kuhusu utumishi wa
Profesa Mahalu?
Mkapa: Namfahamu kama msomi mzuri,
mchapakazi,mhadilifu na kiongozi anayetenda haki.
Mawakili: Mawasiliano kati ya Serikali na Balozi
yanafanyika kwa njia zipi?
Mkapa: Balozi anaweza kuwasiliana na serikali
yake kwa njia ya Barua kwa Wizara ya Mambo ya Nje,Katibu Mkuu Kiongozi,rais au
kwa njia ya mdomo.Na mawasiliano siyo lazima yafanyike kwa njia ya maandishi tu
kwasababu maelekezo mengine ambayo anapewa balozi na serikali yake ni ya siri
kwa maslahi ya taifa hivyo anaweza kuitwa nyumbani na kupatiwa maagizo hayo
kwanjia ya mdomo.
Mawakili: Kwa wadhifa wako ule wa urais,kabla ya
kwenda kuzindua jengo hilo Januari 23 mwaka 2003, hukuwai kupokea taarifa toka
ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP za kukukataza usiende kuzindua jengo
hilo kwasababu kwasababu kuna harufu za ubadhilifu wa fedha za umma?
Mkapa: Ofisi hizo hazikuwahi kunipatia taarifa
hizo.
Yafuatayo ni
mahojiano baina ya mawakili wa serikali Ben Lincoln, Vicent Haule na Ponsian
Lukosi dhidi ya Rais Mkapa:
Mawakili: Ebu ieleze Mahakama ni kwanini bei za
jengo zinatofautiana maana risiti ya manunuzi ya jengo hilo zinaonyesha jengo
lilinuliwa kwa Euro milioni 3 na Ansard ya bunge iliyosomwa na Kikwete bungeni
mwaka 2004 inasema jengo lilinuliwa kwa Shilingi bilioni 2.9?
Mkapa: Kazi yangu siyo kufanya uthamini wa fedha
za kigeni kwamba wakati huo hizo Euro Milioni 3 zilikuwa na thamani gani kwa
fedha Tanzania. (Watu wakacheka).
Mawakili: Nani aliagiza upelelezi wa manunuzi ya
jengo la Italia ufanyike?
Mkapa: Sijui.
Mawakili: Uchunguzi wa jengo hilo ulifanyika wakati
wewe ukiwa madarakani ?
Mkapa: Sijui, milikuja kuona Balozi Mahalu
kashtakiwa mwaka 2007 nikiwa tayari nimestaafu.Siku ya kwanza ya kwanza
alipofikishwa kortini na keshi yake nilithibitisha taarifa hizo kupitia vyombo
vya habari kuwa ni kweli Mahalu ameshtakiwa.
Mawakili: Nani alikupa taarifa za muuzaji wa jengo
hilo anataka kulipwa kwa mtindo huo wa akaunti mbili?
Mkapa: Ni Mahalu na alinipa taarifa kwa mdomo na
alikuwa ameandaa ripoti juu ya ununuzi na akawa anaomba ridhaa ya serikali na
aliomba ridhaa ya serikali kabla ya kununua jengo.
Mawakili: Ulisema hukuweza kuzuia ununuzi wa jengo,
Je ulikuwa na madaraka ya kuweza kuzuia lisinunuliwe?
Mkapa: Eh! Mimi ndiye nilikuwa rais wa nchi
nilikuwa na madaraka pia ya kuzuia serikali isitoe fedha kununua hilo jengo na
badala yake fedha hizo zielekezwe kwenye mahitaji mengine ila kwasababu
nilikuwa ninajua umuhimu na faida ya nchi kununua jengo lile ndiyo maana
nikaridhia kwa mdomo jengo lile linunuliwe.
Wakili: Ulitoa maelekezo kwa nani?
Mkapa: Nilitoa maelekezo jengo linunuliwa kwa
njia yam domo kwa watendaji na maagizo hyo yalipaswa yatekelezwe na wizara ya
Mambo ya NJe na ilikuwa jukumu la Mahalu la kuieleza wizara hiyo na ubalozi
watekeleze maagizo yangu.
Wakili: Kwa hiyo unaieleza mahakama kuwa wizara
ya Mambo ya Nje, ilituma malipo kwa mtindo wa akaunti mbili tofauti?
Mkapa: Ina husu nini sasa?mimi nilitoa maagizo
kwa Mahalu jengo linunuliwe hivyo ni jukumu la balozi mahalu kuieleza wizara
yake sasa suala la hayo makaratasi ya kufanya mchakato wa kulinunua jengo
hilo,mimi kama rais siwezi kuingilia. Nilitoa maelekezo kwa watendaji,watendaji
walipaswa watekeleze.
Mawakili: Utajisikiaje yule muuzaji aliyetuuzia
jengo kuwa uamuzi wake wa kutuuzia jengo kwa mtindo wa akaunti mbili ,alikuwa
akikwepa kodi kwa serikali ya Italia?
Mkapa: Aaah! Misioni tatizo kikubwa hapa
Tanzania tumepata jengo lengo, Aliamundulai. (watu wakacheka).
Mawakili: Ujisikiaje ukisikia Mahalu alitumia zile
Euro milioni tatu zilizonunulia jengo kwa matumizi yake binafsi?
Mkapa: Nitashangaa sana. Pia wewe wakili wa
serikali ndiyo nitakushangaa zaidi kwani Ansard ya bunge iliyosomwa na Kikwete
bungengi imetamka bayana kuwa serikali ilimlipa muuzaji wa jengo na kwamba
taratibu na sheria ya manunuzi ya umma zilifuatwa na kwamba hadi sasa huyo
muuzaji hajawahi kujitokeza kulalamika kuwa hajalipwa fedha zake.
Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa ushahidi wa
Mkapa ambapo Hakimu Mugeta aliairisha kesi hiyo hadi leo ambapo mshtakiwa wa
pili ambaye alikuwa ni Meneja wa Utumishi na Utawala wa Ubalozi huo, Grace
Martin ataanza kujitetea.
Mkapa akaondoka saa 7:29 mchana ndani ya
chumba cha mahakama huku akiwa akiongozwa na walinzi wake zaidi ya watato ambao
walimuongoza hadi nje ya viwanja vya Mahakama hiyo na kupanda gari ambapo
aliondoka kwa msafara ambao uliongozwa na pikipiki iliyokuwa ikilia king’ora
iliyokuwa ikiendeshwa na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani .
Habari ni kwa hisani ya Happiness Katabazi.
Mwandishi wa magazeti yenye kumilikiwa na kampuni ya Free Media
Company.
Ni mmiliki na mwendeshaji wa blog ya Fukuto la Jamii.
No comments:
Post a Comment