CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeruhusu wananchi kuamua kuhusu masuala ya
madaraka ya Rais na uteuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi.
“Sisi CCM tumeona suala hili tuwaachie wananchi walijadili na kuamua wenyewe wanaona Rais apewe madaraka ya aina gani. Ni fursa yao kupendekeza apunguzwe, aongezwe madaraka au madaraka yake yaweje,” amesema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Katika eneo la Tume Huru ya Uchaguzi, Nape amewaeleza waandishi wa habari kuwa, eneo hilo limekuwa gumzo hasa nyakati za uchaguzi huku malalamiko mengi yakiegemea katika utaratibu uliotumika kuteua wajumbe wa Tume hiyo.
Amesema, mapendekezo hayo yaliamuliwa katika semina ya wajumbe wa NEC kuhusu mchakato wa Katiba mpya iliyomalizika hivi karibuni Dodoma.
“Chama kimeona suala hilo lijadiliwe na wananchi na wapendekeze utaratibu mwafaka wa kuteua Tume Huru ya Uchaguzi,” alisema Nape.
Alitaja masuala mengine ambayo chama hicho kimeona wapewe wananchi fursa ya kuchangia maoni yao kwa kuzingatia maslahi ya nchi na ikiwezekana yabadilishwe, kuwa ni masuala yanayosababisha kero za Muungano na utaratibu wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Alitaja pia maeneo ya kujadiliwa kuwa ni eneo la uteuzi wa mawaziri, waziri mkuu, muundo wa Bunge, Baraza la Wawakilishi na aina ya wabunge na wawakilishi.

Ametaja maeneo mengine kuwa ni, kuhoji mahakamani matokeo ya uchaguzi
wa Rais na mgombea binafsi.
“Kuna watu wanadhani kuwa CCM inaogopa mgombea binafsi, si kweli,
hatuna tatizo na hilo na ndiyo maana tumeliweka hili watu walijadili na
kuamua watakavyo, ingawa kwa mtazamo wangu, mgombea binafsi ni kitanzi
kwa upinzani,” alisema.
Alitaja maeneo mengine kuwa ni uwepo wa Baraza la pili la Kutunga Sheria, ukomo wa idadi ya wabunge, nafasi ya Rais wa Zanzibar katika uongozi wa Serikali ya Muungano na mfumo wa Mahakama.

No comments:
Post a Comment