Wednesday, May 9, 2012

Cheka kimya kimya

Siku ya kufunga shule mzazi mmoja kaenda na mwanae shule, sherehe zikaanza wanafunzi wakawa wanapewa vyeti na zawadi kadri ya ubora kwenye masomo, mtoto wa jamaa yetu hakutajwa hata jina; 
Baba: Wale ndiyo watoto, mbona Mungu kaninyima? 
Wakaondoka na kuelekea kituo cha basi kuwahi basi la kwenda kwao. 
Wakati huo huo wazazi kadhaa wenye magari wakawa wamekuja kuwachukua watoto wao;
 
Mtoto: Dah wale ndiyo wazazi, mbona Mungu kaninyima!
 Chanzo: John Kitime kwenye facebook

No comments:

Post a Comment