Wednesday, May 9, 2012

Basi lateketea kwa moto Morogoro




Basi la Kampuni ya  Muro Investment, lenye namba za usajili, T820BEY lililokuwa likitoka Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea  kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro. 
Ajali hiyo iliyotokea jana (Mei 8,2012) saa 1:15 usiku,  haikusababisha madhara kwa abiria ila mali zao zote ziliteketea.

 Mmoja wa wahusika katika basi hilo alidai kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme kwenye gari hilo.
Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto.
 Magari yakipita pembeni ya basi hilo lililokuwa likiteketea kwa moto na hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuuzima hivyo gari hilo liliteketea kabisa.
Mashuhuda.

Kwa hisani ya blog ya Father Kidevu

No comments:

Post a Comment