Mtoto wa ajabu amezaliwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, mjini Songea, maumbile yake
ya sehemu za siri yako kichwani.
Tanzania Daima limeshuhudia tukio hilo la mtoto huyo ambaye
amehifadhiwa katika chumba cha uangalizi maalumu katika hospitali hiyo,
kwa lengo la kujaribu kupunguza msongamano wa watu ambao wamekuwa
wakimiminika kumshuhudia.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Mathayo Chanangula, alisema
mtoto huyo alizaliwa Aprili 25, mwaka huu, saa saba mchana akiwa na
uzito wa kilo 1.9 licha ya kutimiza miezi tisa ya kuzaliwa.
Chanangula lifafanua kuwa kwa kawaida mtoto anatakiwa kuzaliwa na
uzito wa kilo 2.5.
Pia alieleza sababu za kitaalamu zilizosababisha
mtoto huyo kuzaliwa katika hali hiyo kuwa ni unywaji wa dawa
zisizostahili kwa mama mjamzito kabla ya kutimiza miezi mitatu ya
ujauzito.
Mtoto huyo kila anaponyonya, sehemu hiyo za siri ya jinsia ya kiume
iliyo kichwani kwake inasimama kama vile anataka kujisaidia haja ndogo.
Naye muuguzi mkunga wa hospitali hiyo, Philomena Mwingira, alisema
mtoto huyo amezaliwa akiwa na maumbile yasiyo ya kawaida, hivyo hawawezi
kumuacha nje badala yake wameamua kumhifadhi katika chumba maalumu na
kwamba wanaendelea kumfariji mama huyo kukubaliana na hali hiyo.
Wazazi wa mtoto huyo, Stumai Ausi na Abdallah Saidi, wakazi wa
Msamala mjini Songea, wameiomba jamii na wataalamu mbalimbali kuwasaidia
kumaliza tatizo la mtoto wao ili aweze kurejea katika maumbile yake ya
kawaida.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment