SAKATA la kujitokeza kwa wanawake wanaodai kuzaa na aliyekuwa msanii wa filamu nchini, Steven Kanumba, limezidi kushika kasi baada ya mwanamke mwingine Paskalia Macha (20) mkazi wa kitongoji cha Bangwe mjini hapa kudai kuzaa na msanii huyo.
Alidai kuwa Johnson alizaliwa katika hospitali ya Mwananyamala Desemba 18, 2008, lakini alipomjulisha Kanumba alimjibu kuwa hiyo ni zawadi pekee aliyomwachia maishani.
Mwanamke huyo amevuta hisia za wakazi wengi mjini hapa alipojitokeza hadharani na kudai kuwa mtoto wake wa kiume aliyemzaa miaka mitatu na miezi minne iliyopita, baba yake mzazi ni Kanumba aliyefariki dunia hivi karibuni.
Kanumba alikufa usiku wa kuamkia Aprili 7 na kuzikwa siku tatu baadaye kwenye makaburi ya Kinondoni.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi nyumbani kwa mama yake mzazi, Virginia Makungu (69) alimtaja mwanawe huyo kuwa ni Johnson Steven Kanumba. Paskali ambaye kwa sasa anaishi kinyumba na Giles Mtula (27) mwoka mikate tangu mwaka jana, tayari ana mtoto mwingine wa kike aitwaye Vero mwenye umri wa mwezi mmoja.
Alidai kuwa Johnson alizaliwa katika hospitali ya Mwananyamala Desemba 18, 2008, lakini alipomjulisha Kanumba alimjibu kuwa hiyo ni zawadi pekee aliyomwachia maishani.
Akihadithia mlolongo wa maisha yake, alidai kuwa hakuhitimu elimu ya msingi kwani aliishia darasa la tano na kwa ridhaa ya mama yake mzazi, alimkabidhi kwa mwanamke aishie Dar es Salaam kufanya kazi za ndani, lakini tajiri wake huyo ambaye hakutaka kumtaja jina alimpeleka kufanya kazi ya baa Mtoni Mtongani.
Alidai kuwa kazi ya baa ilimshinda, hivyo akiwa na mhudumu mwenzake wake kike walitoroka na kujihifadhi kwa msamaria mwanamke mwingine aliyekuwa akiishi Gongo la Mboto na kuwa mfanyakazi wake wa ndani.
Habari zingine zilidai kuwa akiwa anafanya kazi katika baa ya Mtoni Mtongani alianza uhusiano na Kanumba. “Alijitambulisha kwangu kuwa Steven Kanumba mwenyeji wa Shinyanga … nilianza naye uhusiano kimapenzi mwaka 2006 nikiwa msichana mdogo wa miaka 14 na alikuwa akinifuata mara kwa mara Gongo la Mboto na mwaka 2008 nilipata ujauzito wake.
“Hakunilazimisha kufanya naye mapenzi bali nilimkubalia kwa hiyari yangu mwenyewe,” alisema. Lakini kwa uchungu mkubwa alidai kuwa alipomfahamisha kuwa ana ujauzito Kanumba aliukana kuwa hahusiki kwa lolote na ujauzito huo, ila kama ni kweli basi ni zawadi maalumu kwa maisha yake yote.
“Kaka yangu alikuja Dar es Salaam na kunirudisha Sumbawanga kwa mama yangu mzazi wakati huo mwanangu alikuwa na umri wa miezi sita nilipofika tu mama yangu mzazi aliponiuliza nimezaa na nani sikumficha, nilimweleza wazi kuwa baba wa mtoto ni Kanumba, lakini amemkataa. “Mama alinitunza na mjukuu wake hadi mwaka jana nilipoanza kuishi kinyumba na Giles … sasa tuko katika mipango ya kumbatiza maana mimi ni Mkatoliki,” alisema.
Paskalia alidai kuwa ndugu zake wote akiwamo mumewe, aliwafahamisha baba wa mtoto huyo tangu Kanumba akiwa hai. Hivi sasa anaomba ndugu wa marehemu waje Sumbawanga wamchukue mtoto wao, kwani anadai ni damu yao halali, ili wamsomeshe kwa kuwa hana uwezo wa kumsomesha.
“Ninachotaka ni ndugu zake waje wamwone mtoto huyu, ni damu yao halali, wamsomeshe …kama wana shaka niko tayari mwanangu afanyiwe vipimo vya vinasaba ili ninayosema yajidhihirishe,“ alisema.
Giles alipohojiwa alikiri kuishi kinyumba na Mama Johnson tangu mwaka jana na kwamba alipoanza uhusiano naye, alimweleza bila kumficha kuwa baba mzazi wa Johnson ni Kanumba.
“Mie mtoto huyu namfahamu kama Johnson Steven Kanumba mtoto wa msanii maarufu nchini, kwanza sikuamini kabisa lakini nilianza kuamini, kwani kama mara mbili hivi Kanumba alikuwa akimpigia simu mke wangu akisisitiza kuwa hayuko tayari kutoa matumizi yoyote kwa Johnson ila eti amempa kama zawadi yake mke wangu.
“Mara ya mwisho ilikuwa siku mbili hivi kabla hajafikwa na mauti, kauli ambayo imewachukiza baadhi ya ndugu wa mke wangu, wakiichukulia kauli hiyo kuwa ni matusi kwao.
“Mke wangu alilia sana baada ya kujulishwa kuwa baba wa Johnson ni marehemu, kwa kweli aliomboleza kivyake haikuwa rasmi … mie binafsi naamini Kanumba ni baba mzazi wa Johnson,” alisema baba wa kambo wa Johnson. Mama mzazi wa Paskalia alikiri kuwa binti yake alimweleza kuwa baba wa mtoto huyo ni Kanumba ambaye baadaye alianza kumwona kupitia filamu alizoigiza.
“Mjukuu wangu Johnson ni mkimya sana wakiwapo wageni, lakini wakiondoka huwa anaigiza yote, nadhani ana kipaji cha kuigiza kama marehemu baba yake.
“Tulipigwa na butwaa siku moja kabla ya kufariki dunia kwa baba yake, kwani ilipofika jioni, ghafla alilia huku akigaragara chini mbele yangu akimtaja baba yake … ndipo kesho yake tukasikia kupitia vyombo vya habari kuwa baba yake amefariki dunia.” Alisema yeye na wanafamilia wote wako tayari mjukuu wake huyo afanyiwe vipimo vya kitaalamu ili ukweli ujulikane.
“Mie sikubali mjukuu wangu tumpeleke Dar bali hao ndugu zake waje huku ili tukubaliane maana sitaruhusu wamchukue mpaka wanilipe fidia kwa mila za Kifipa kuna malipo ya mama kwa kuwa ameshamwaribu binti yangu, pia kwa kuwa nimemtunza mtoto wao, lazima wanilipe, ila siko tayari kusema ni kiasi gani ni mambo ya kujadiliana na kukubaliana,” alisema.
Johnson alipoulizwa jina la baba yake alitaja Steven Kanumba hata alipooneshwa picha ya marehemu na kutakiwa amtambue ni nani kwa mastaajabu ya wengi alimwonesha akisema, “huyu ni baba yangu.”
Ndugu wakiwamo kaka za mama wa Johnson walikiri kwamba aliwajulisha kuwa baba mzazi wa Johnson ni Kanumba mara aliporejea hapa mtoto huyo akiwa na umri wa miezi sita.
“Kwanza sikuamini baadaye nilipobaini kuwa baba wa Johnson ni Steven Kanumba mwigizaji maarufu wa filamu nilipokuwa nikimwona akiigiza katika runinga. Dada (Paskalia) alinijulisha hayo mwaka 2010,“ alisema Humphrey Kalulu (16) mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Sekondari ya Chanji mjini humo, ambaye alijitambulisha kuwa ni binamu wa Paskalia.
Hata hivyo, baadhi ya ndugu wa Paskalia akiwamo binamu yake aitwaye Godfrey Makungu, hawako tayari ndugu wa Kanumba kumchukua Johnson kwa kile wanachodai kuwa marehemu katika uhai wake alimkana mtoto huyo hivyo walikwenda mbali hata kumlazimisha Paskalia akatae Kanumba kuwa baba mzazi wa Johnson.
Habari za ndani kutoka familia hiyo zilidai kuwa baadhi ya ndugu wa Paskalia wakiongozwa na Godfrey, waliandaa mipango ya kumpeleka Paskalia na Johnson Namanyere wilayani Nkasi wakaishi huko ikiwa ni jitihada za kumficha mtoto huyo ili asichukuliwe. Wakazi wengi wa hapa na kwingineko wamekuwa na maoni tofauti, wengi wakitaka mtoto huyo afanyiwe vipimo vya vinasaba .
“Miye naomba ndugu wa marehemu Kanumba waje wamshuhudie mtoto huyu kwa kweli anafanana na baba yake, ili kama wana shaka basi vipimo vya DNA vitumike kubaini haya … maana limekuwa kwa wengine kama fumbo, basi ni lazima liteguliwe kama ni kweli basi wasimnyime ndugu yao fursa ya kumpa elimu, “ alisema Afred Manyika, mfanyabiashara maarufu mjini hapa.
Chanzo: Gazeti la HabariLEO
I was recοmmended this wеb site by
ReplyDeletemy cousin. I'm not sure whether this post is written by him as nobody else know such detailed about my difficulty. You are wonderful! Thanks!
Here is my web site ... payday
my website :: payday
Goοd sitе yоu have got heгe.
ReplyDelete. It's hard to find quality writing like yours nowadays. I seriously appreciate people like you! Take care!!
Check out my web site - New Bingo Sites