KUNA taarifa kwamba mgomo wa madaktari umeanza rasmi nchi nzima.
Madaktari leo wametangaza kwamba, wameanza mgomo rasmi hadi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya watakapojiuzulu au kuondolewa kwenye nyadhifa zao.
Kwa mujibu wa madaktari hao, walipozungumza na Serikali wakati wamegoma wiki kadhaa zilizopita, walikubaliana mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kwanza, uongozi wote wa juu wa Wizara ya Afya uondolewe, lakini hadi sasa makubaliano hayo hayajatekelezwa.
Wamesema, hawawezi kuendelea na mazungumzo na Serikali wakati makubaliano ya kwanza hayajatekelezwa.
Madaktari wamesema, hawawezi kuendelea kusubiri kutekelezwa kwa makubaliano hayo, na kwamba, utekelezaji wake hauhitaji kusubiri kwa kuwa, hauhitaji bajeti.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alisema, masharti ya madaktari ya kutaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk . Hadji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya waondolewe nyadhifa zao ndipo majadiliano mengine yaendelee, hayakubaliki.
No comments:
Post a Comment