Monday, March 5, 2012

Buriani Jane Mponzi, msalimie Herry

Herry Makange na Jane Mponzi siku ya sherehe ya send off ya Jane miaka kadhaa iliyopita. (Picha kwa hisani ya blog ya Mroki)



Meshack Nzowa wa Radio Magic FM/ Channel Ten jana alinipigia simu kunipa taarifa ya kifo cha shemeji yetu, Jane Mponzi.



Nilimdadisi Nzowa anieleze sababu ya kifo cha Jane, akanieleza kwamba alipata shinikizo la damu (presha), akapelekwa hospitali, kwa bahati mbaya haikuwezekana kuokoa maisha yake, amekwenda, katangulia.



Baada ya kumaliza kuzungumza na Nzowa, niliwaza mambo mengi, nilimkumbuka zaidi Herry Makange, hasa kwa kufananisha mazingira ya vifo vyao.



Herry alikufa kwa ajali, Dar es Salaam miaka michache tu baada ya kufunga ndoa na Jane.



Jane anatarajiwa kuagwa kesho mchana nyumbani kwao Oysterbay jijini Dar es Salaam, atazikwa Machi 7 mkoani Iringa.


Poleni sana wafiwa wakiwemo wazazi wa Jane, mwanawe, Melanie, ndugu jamaa na marafiki wakiwemo wafanyakazi wenzake, Vodacom.


Buriani shemeji Jane, umemaliza safari yako, pumzika kwa amani.

No comments:

Post a Comment