Thursday, July 21, 2011

Pinda- Serikali haijashindwa kumaliza mgawo

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma, muda mfupi baada ya mtoto huyo wa mkulima kuapishwa kumrithi Edward Lowassa katika madaraka hayo.



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, leo amelieleza Bunge kuwa, Serikali haijashindwa kumaliza tatizo la mgawo wa umeme.



Pinda ametoa msimamo huo wakati anajibu maswali ya papo hapo bungeni mjini Dodoma.



Mgawo wa nishati hiyo muhimu limekuwa ni tatizo sugu kwa miaka kadhaa sasa na kwa mujibu wa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, unatarajiwa kwisha baada ya miezi 18 kuanzia sasa.


Pinda amewaeleza wabunge kuwa, si kweli kuwa Serikali imeshindwa kumaliza mgawo wa umeme, inahitaji muda, na ikishindwa iumbuliwe bungeni.



Wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini, wabunge walisema, wamechoka kusikia orodha ya miradi ya kuzalisha nishati hiyo, wanataka umeme.



Tatizo la umeme lilisababisha Edward Lowassa ajiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008, kwa sababu ya kashfa ya Richmond.



Waziri Ngeleja anashinikizwa ajiuzulu kwa madai kuwa Wizara imemshinda, amekataa.

No comments:

Post a Comment