MIGOMO na maandamano bado inazidi kukiandama Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), muda mfupi uliopita, Chuo Cha Sanaa, Lugha na Sayansi ya Jamii katika chuo hicho kimefungwa leo, wanafunzi wote wameamriwa kuondoka.
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rubagumya leo saa nne asubuhi ametangaza kufungwa kwa chuo hicho na haijulikani lini kitafunguliwa.
Polisi wapo maeneo ya chuo, ifika saa nane mchana leo wanafunzi wote wa chuo hicho wanatakiwa wawe wameondoka katika eneo la chuo.
Inadaiwa kuwa sababu ya mgogoro katika chuo hicho ni shinikizo la wanafunzi kutaka wakafanye mafunzo kwa vitendo.
Wanafunzi walikuwa wamegoma tangu juzi, leo asubuhi wakaandamana kwenda kwa Mkuu wa chuo, ndipo akatangaza kuwa kimefungwa.
Hivi sasa wanafunzi wapo kwenye pilika za kuchukua mizigo yao kuondoka chuoni.
Mgomo haukuanza jumatatu kama inavyoripotiwa, mgomo ulianza ijumaa trh 10 june baada ya kubandikwa kwa tangazo la kutokuwepo field trh 09 june. Pia leo wanafunzi hawakuandamana kwenda kwa mkuu wa chuo Hon B W MKAPA au makamu wake PROF KIKULA bali waliandamana kwenda kwa principal wa college SSH prof RUBAGUMYA. Naomba kuwasilisha
ReplyDelete